Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu nchini kuanzia Mei 10 hadi 12 mwaka huu.
Katika ziara hiyo Rais Zuma ataambatana na mawaziri sita pamoja na wafanyabiashara 80 ambao watakuja wa ajili ya sekta ya biashara.
Rais Zuma atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, Rais John Magufuli na baadae kufanya mazungumzo ya pamoja kati ya ujumbe wa Afrika Kusini na ujumbe wa Tanzania.
Akizungumzia ziara hiyo waziri wa Mambo ya nje ya Nchi, Balozi Augustino Mahiga amesema kuwa serikali ya Tanzania na Afrika Kusini zitatiliana saini mikataba 10 kwenye sekta za biashara, Uwekezaji, Miundombinu, Utalii na Nishati.
Waziri huyo amesema kuwa nchi za Tanzania na Afrika Kusini zimeamua kutumia uhusiano wa kihistoria kama kuanzisha uhusiano mpya wa kiuchumi kwa kuongeza uwekezaji.
Katika ziara hiyo Zuma atashiriki mkutano wa wafanyabiashara, atazindua jengo la ubalozi wa Afrika Kusini na kutembelea taasisi ya moyo ya Jakaya Kiwete.