Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameamriwa kufika mahakamani wiki ijayo kukabiliana na mshtaka mbalimbali ya rushwa ambayo yana thamani ya mabilioni ya Dola za Marekani.

Mwanasheria wa Zuma ameeleza kuwa Zuma alipewa jana taarifa rasmi ya kufika kwenye Mahakama Kuu ya mji wa Durban April 6, 2018.

Kesi hiyo inahusiana na jukumu lake katika mpango wa silaha za miaka ya 1990.

Waendesha mashtaka mara ya kwanza walimshtaki Zuma kuhusu kesi hiyo mwaka 2005 kipindi akiwa Makamu wa Rais.

Lakini mashtaka haya yalifutwa wiki chache baada ya kuwa Rais wa nchi hiyo kwa madai kwamba, mashtaka hayo yalikuwa yana shinikizo la kisiasa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *