Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook, Mark Zuckerberg ametoa maelezo katika Bunge la Marekani- Congress kwa mara ya kwanza Jumanne, akijibu wasiwasi ulioelezwa na wabunge juu ya kushindwa kwa mtandao wa jamii maarufu kulinda taarifa zao.
Taarifa hizo za siri ni za watumiaji wanaofikia milioni 87 ulimwenguni zilizotumiwa na kampuni yenye kujishughulisha na siasa- Cambridge Analytica iliyokuwa na mafungamano na Trump.
Mahojiano hayo yanaendelea Jumatano wakati Zuckerberg atakapokutana katika raundi ya pili kujibu maswali mbele ya jopo la Wabunge wa Marekani.
Wachambuzi wanasema ni kosa ambalo liliruhusu kampuni ya kisiasa ya Cambridge Analytica kupata taarifa kwa kupitia programu iliyotengenezwa na kampuni nyingine, ambayo ili ingilia taarifa binafsi za mamilioni ya wanaotumia Facebook duniani.
Marc Rotenberg wa kituo cha kutunza taarifa za siri za kielektroniki amesema: “Ni suala nyeti kwa Facebook kwa njia nyingi. Kuhakikisha bei ya hisa zao zinanyanyuka, watu wana wasiwasi mkubwa juu ya mustakbali wa kampuni hiyo. Lakini nafikiri vipi Facebook itaweza kuendelea kufanya shughuli zake kama ilivyo kwani ni suala la wazi. Nafikiri mjini Washington na maeneo mengine, utashuhudia shinikizo la kuwepo mabadiliko ya kweli.
Mabadiliko yaliyoanza katika mahojiano yasiyo ya kawaida kabisa yakiendeshwa na nusu ya Baraza la Seneti ya Marekani.