Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu amefunguka na kusema kuwa yeye kama mwanamke hawezi kukwepa kutongozwa na wanaume licha ya umaarufu wake.

Zuchu amesema kuwa mara nyingi akiandika nyimbo amekuwa anawaza mama akisikia huu mstari atanifuta kwenye mirathi.

Lakini mama yake Khadija Kopa ni muelewa anajua kazi nnayoifanya na mimi ni mtoto mzuri sio mcharuko hivyo anajua ninajielewa na ninajua ninachokifanya.

Amesema kuwa “Mimi ni mtoto mzuri sana na muda mwingine nyimbo zangu zinanifanya nisiwe comfortable, lakini sitengenezei muziki wa watoto tu natengenezea na watu wazima pia wasikilize kwenye starehe zao.

Pia amemaliza kwa kusema “Ukiwa msichana huwezi kukwepa kutongozwa, lakini ni wewe unavyojibeba. Ukiwa na kipaji na umetulia unajielewa utachukuliwa serious lakini ukirembesha sauti kutafuta njia zingine za kupata mpenyo utaingia kwenye line.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *