Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu ameingia kwenye Top 10 ya BBC pamoja na wasanii wengine Afrika wanaopaswa kutazamwa zaidi 2021.

Mwanamuziki huyu huimba kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza na ana sifa za muziki wa Tanzania aina ya Bongo Fleva. Mwaka uliopita msanii huyu alitoa albamu yake ya uzinduzi I AM Zuchu na pia aliingia kandarasi na Lebo ya kurekodi muziki ya WCB Wasafi.

Kulingna na programu ya kucheza muziki ya Boomplay , Albamu yake ndio iliochezwa sana nchini Tanzania mwaka 2020 na video za muziki wake zimefanikiwa kuvutia mamilioni ya mashabiki katika mtandao wa You Tube.

Fik Fameica (Uganda)

Fik Fameica, ambaye pia anajulikana kama Fresh Boy, ni mmojawapo wa wanamuziki wa muziki wa aina ya Rap waliovutia wengi kutoka Afrika mashariki kwa sasa. Mara ya kwanza mwanamuziki huyo alipanda katika ulingo wa muziki 2017 akicheza muziki wake Kutama.

Kijana huyo hapigi muziki kama ule unaochezwa na wasanii wengine nchini Uganda na yeye hupiga muziki ambao umeshawishiwa na muziki wa rege.

Gaz Mawete (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo)

Gaz Mawete alianza muziki 2018 kwa kutumia aina ya muziki ya Olingi Nini, na alipanda na kuwa maarufu duniani kwa kupiga muziki wa Kifaransa.

Mchezaji densi huyo wa Dr Congo , ambaye alijipatia umaarufu nyumbani baada ya kushiriki katika mashindano ya kusaka vipaji amepiga kolabo na fally Ipupa ambaye alionekana katika wimbo a C’est Rate.

Kabza De Small (Africa Kusini)

Kabza De Small amevutia wengi tangu alipoanza kuachilia muziki wake 2016.

Dj huyo na mzalishaji wa muziki amepewa jina la utani la kuwa mfalme wa Amapiano, aina moja ya muziki nchini Afrika kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *