Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu kutoka WCB ameibua gumzo na shangwe kwa baadhi ya wafuasi wake baada ya kudai anajisikia uvivu mno na kulala muda wote.
Miezi kadhaa iliyopita, Zuchu alihusishwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na bosi wake wa Lebo ya WCB, Diamond Platnumz ingawa wote wamekuwa wakikanusha jambo hilo.
Zuchu amesema; “Najisikia mvivumvivu leo, nalala ovyo…”
Kauli hiyo ya Zuchu imewaibua wataalam wa mambo hayo ambao wamedai kwamba huwenda Zuchu amenasa mimba ya Diamond au Mondi.
Wataalam hao wanasema kuwa uchovu na kujisikia kulalalala ni dalili za mwanzo za mwanamke mwenye mimba changa.
Wanasema kuwa, uchovu huo wa Zuchu si bure na kwa vyovyote kutakuwa na kitu huku baadhi ya watu wakidai bora isiwe kweli kwa sababu Simba hachelewi kumpiga chini na kujikuta akilea mwenye kama ma-baby mama wake wengine.