Mwanamuziki wa Bongo Fleva, kutokea lebo ya WCB, Zuchu amefikia Subscribers Milioni moja kwenye chaneli yake Ya YouTube.
Zuchu anakuwa mwimbaji wa kwanza wa kike Tanzania kufikia idadi hiyo ya Subscribers kupitia chaneli yake kwenye mtandao huo ndani ya muda wa miezi michache.
Hata hivyo Zuchu kwenye chaneli yake hiyo kazi zake zimetazamwa zaidi ya mara milioni 140 mpaka sasa tangu alipopakia kazi yake ya kwanza Miezi 11 iliyopita.
Aameweka rekodi mpya Afrika Mashariki na kati kwa kuwa msanii wa kike wa kwanza kufikisha Subscribers Milioni Moja YouTube na wa pili kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara
Zuchu ametimiza idadi hiyo akiwa nyuma ya Yemi Alade mwenye Subscribers Milioni 1.7. Zuchu staa kutoka lebo ya WCB amekuwa kati ya wasanii wachache Afrika wanaokuwa kwa kasi kwenye soko la muziki Duniani
Mwanamuziki huyo amewashukuru mashabiki wake kwa kufikia idadi hiyo ya wafuasi kwenye mtandao huo. Kupitia Instagram akaunti yake baada ya kufikisha wafuasi.