Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zary The Boss Lady amefunguka na kusema kuwa yeye sio shabiki wa mwanamuziki licha ya kuzaa naye watoto wawili.
Mara tu baada ya kutua Tanzania kwa ziara ya kikazi, Zari amesema kuwa kuna mengi ambayo hufanyika kati yake na Diamond au Mondi bila kutangaza.
Alieleza kuwa yeye na Diamond hujadialiana kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu ikiwamo namna ya kulea watoto wao wawili pamoja.
“Mimi kuonana na Diamond ama familia yake siyo lazima iwe kwenye vyombo vya habari, tumeshakuwa familia, mimi naongea na Diamond kila wakati kuhusu watoto na jinsi ya kuwalea.
“Siyo lazima nikikutana naye niposti, mimi siyo shabiki wake, mimi ni mama wa watoto wake,” anasema Zari.