Mzazi mwenzake na Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady amevunja ukimya baada ya kusema kuwa katika maisha yake ameolewa mara moja katika maisha yake.

Zari amesema kuwa, ndoa pekee aliyofunga ilikuwa kati yake na mumewe, Ivan Ssemwanga ambaye alitangulia mbele ya haki Mei 25 mwaka 2017.

Zari alifahamika zaidi baada ya kuwa mpenzi wa Diamond kisha kuzaa naye watoto wawili, Tiffah na Prince Nillan ambao kwa sasa wanasaidiana kuwalea, kwani waliachana huku Zari akiendelea na maisha yake nchini Afrika Kusini.

Katika mahojiano hayo, Zari anasisitiza kuwa, hawezi kuacha kuishi maisha yake kwa sababu watu watamsema. “Nimeolewa mara moja tu. Wengine wako wamekwama maishani na bahati mbaya, hawana hata mtuanayewauliza.

Zari anasema kuwa, miongoni mwa mambo ambayo hafurahishwi nayo kabisa ni kuhukumiwa,” Anasema Zari.

Hata hivyo, mambo hayo yote yanakuja siku chache baada ya Zari kusema kwamba amechoka kueleza watu kuhusiana na maisha yake mitandaoni.

Pia hii ni baada ya ule uvumi kuenea kwamba ameolewa kwa mara nyingine.“Kuanzia sasa nitaweka kile ninachojisikia, kama kitakukera ni-unfollow, nimechoka kuwa mtumwa wa kujieleza kwa nini nafanya kitu f’lani?”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *