Mfanyabiashara maarufu, Zari The Boss Lady amefunguka kuhusiana na matatizo waliyopitia yeye na mpenzi wake Diamon miezi michache iliyopita baada ya Diamond kuzaa na Hamisa Mobeto.
Miezi michache iliyopita habari hii ilienea kama moto wa kifuu na kusababisha tafrani kwenye mitandao ya kijamii pale Diamond baada ya kukiri kuzaa na Hamisa Mobeto.
Baada ya sakata hilo Diamond na Zari walisameheana na kurudiana lakini tangu siku ile Zari hajawahi kuongelea ishu hiyo wala kueleza chochote kuhusu alivyojisikia mpaka juzi alipofanya mahojiano nchini Uganda.
Zari yupo nchini Uganda sasa hivi akijiandaa na tamasha lake analofanyaga la Zari All White Party litakalofanyika tarehe 21 nchini Uganda.
Katika jitihada za kuitangaza shughuli hiyo anaputa kufanya interview na vituo mbali mbali vya redio.
Lakini Zari amesisitiza kuwa hawezi kumkataza Diamond kumuona mtoto wake aliyezaa na Hamisa kwani mtoto hana kosa lolote ni malaika tu. Pia amesema yeye na Diamond wako vizuri na amebadilika sana.