Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaanza kutoa elimu ya sekondari bila malipo kuanzia mwaka 2018.
Rais Dkt Shein ametoa kauli hiyo mjini Unguja katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha nne na cha sita.
Ameongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa mwaka huu itatoa nafasi 15 za ufadhili wa masomo kutoka nafasi kumi ambazo zilitolewa mwaka jana.
Aidha Rais Dkt Shein ametoa wito kwa wanafunzi watakaopata ufadhili nje ya Zanzibar kurudi nyumbani mara baada ya mafunzo yao ili kulitumikia taifa.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika khafla hiyo wamemshukuru Rais na kuahidi kusoma kwa bidi ili kulitumikia taifa.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd pamoja na vingozi wengine wa serikali visiwani humo.