Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Young Lunya amesainiwa rasmi na lebo kubwa ya muziki Afrika, Sony Music Entertainment Africa Family.

Young Lunya amefanya vizuri katika nyimbo alizoshirikishwa na wakongwe kama Professor Jay, Chidi Benz na Nikki Mbishi na alikuwa memba wa kundi maarufu la OMG kabla hajaachana nalo na kuwa solo artist mwaka 2019.

Young Lunya amesema; “nimetokea kwenye mkoa ambao hata kuzungumzia lebo kubwa ni kama hadithi na ndoto lakini nilipambania kuzifanya ndoto zangu zitokee.

Mwanamuziki huyo kwasasa anaendelea kufanya vizuri kwenye muziki wa hip hop kutokana na ubora wa kazi zake alizofanya toka aanze muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *