Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Young Lunya amethibitisha kusaini lebo ya Rockstar Africa ambayo makazi yake yapo nchini Afrika Kusini.

Young Lunya amethibitisha hilo kupitia akaunti yake ya Instagram kuwa kwasasa atakuwa chini ya lebo hiyo ya nchini Afrika Kusini na sasa atakuwa anasimamiwa na lebo hiyo.

Ameandika “Ninayo Furaha Kuwataarifu Wapenda Burudani kuwa Nimesainiwa Rasmi Na Music Label and Management Company ya Rock Star Africa.

Aprili Mwaka huu Young Lunya alifunga safari kuelekea Mjini Johannesburg Afrika Kusini  kwaajili ya Maongezi na Makubaliano na Lebo hiyo na siku ya leo Yeye pamoja na Lebo hiyo wamethibitisha kuwa Wameanza kufanya kazi rasmi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *