Mwanamuziki wa Rap Bongo, Young Lunya amemtaja Rapper Joh Makini kuwa ni miongoni mwa wasanii walioshirikishwa kwenye album yake mpya ijayo ambayo ameendelea kuipika.

Kupitia ukurasa wa instagram ambaye yupo chini ya usimamizi wa Intersource Records ame-share picha akiwa na mwamba wa kaskazini Joh Makini na kuacha ujumbe usemao “kuna ngoma moja nimeshirikiana na Joh Makini kwenye Abum yangu”.

Hii itakuwa sio wimbo wa kwanza kwa wawili hawa kufanya pamoja kwani Joh pia aliwahi mshirikisha kwenye ‘Mchele’ mwaka mmoja uliopita.

Mwanamuziki huyo ameamua kumshirikisha mwanamuziki huyo ambaye waliwahi kufanya kazi iliyokuwa inaitwa Mchele ya Joh Makini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *