Mwanamuziki wa hip hop Bongo, Young Killer ameachia video ya wimbo uitwao ‘Ngosha’ kama alivyo aahidi kuachia wimbo wake wa kwanza kutoka kwenye album yake ijayo.
Young Killer ambaye ni mzaliwa na mwakilishi wa jiji la Mwanza, anaachia ‘Ngosha’ ukiwa ni wimbo wake wa pili kuaachia sambamba na video kwa mwaka 2022 baada ya ‘Oh My’ aliomshirikisha Mzee Yusuph.
Msodoki ametimiza ahaadi yake hiyo leo April 09 2022, kazi ambayo video yake imeongozwa na Hydro.Inc na audio ya wimbo huo ikitayarishwa na Dapro.
Mwanamuziki huyo ameachia video hiyo baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia wimbo mpaka watu wakaanza kusema kuwa mwanamuziki huyo ameacha muziki.