Kiungo wa Manchester City, Yaya Toure amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja katika klabu hiyo ya ligi kuu nchini Uingereza.

Toure mwenye umr wa miaka 34 alijiunga na klabu hiyo mwaka 2010 akitokea Barcelona na amefunga magoli 81 katika michezo 299 alizocheza katika klabu hiyo.

Mwanzoni mwa msimu huu, Toure aliachwa nje ya kikosi kilichoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa wa Ulaya na kisha kocha wake Pep Guardiola akaingia kwenye malumbano na Dimitri Seluk ambaye ni wakala wa mchezaji huyo.

Kwa siku za hivi karibuni Toure ameibuka na kuwa muhimili wa klabu hiyo jambo lililomfanya Guardiola kumuongezea mkataba mwingine.

Klabu hiyo ya Manchester City imejipanga kufanya mambo makubwa baada ya kufanya usajiri wa mchezaji Bernado Silva kutoka Monaco ya Ufaransa.

Pep Gurdiola ameonekana kuimarisha kikosi chake kutokana na kufanya vibaya kwa msimu uliomalizika huku akiambulia nafasi ya tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *