Kiungo wa Manchester City, Yaya Toure amekubali kosa lililokuwa linamkabili la kuendesha gari akiwa amelewa huku akisema hakutumia pombe kwa makusudi.

Toure amekamatwa Desemba 3 jijini London baada ya kuzuiwa na maafisa wa polisi wakati akiendesha gari na baada ya vipimo ilidaiwa kuwa Toure alikuwa ametumia pombe.

Toure amesisitiza kuwa yeye ni muumini mzuri wa dini ya kiislam anayefuata sheria za dini yake hivyo hatumii pombe na mara nyingi amekuwa akikataa kunywa champagne mara zote anapoibuka ‘Man Of The Match’.

Kiungo huyo amesema kuwa ‘Kuendesha gari ukiwa umelewa ni kosa kubwa na mimi nalifahamu hilo na sikutumia pombe makusudi, nalikubali kosa na faini lakini  napenda kuomba msamaha kwa hili’.

Pia ameongeza kuwa ‘Napenda pia kuwashukuru familia yangu, uongozi na wafanyakazi wote wa Manchester City, wanasheria wangu na mashabiki kwa  msaada wao walionipa katika wakati huu mgumu’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *