Klabu ya Yanga imeshindwa kutamba uwanja wa nyumbani baada ya kutoka 1-1 na timu ya Ngaya kutoka Comoro kwenye mechi ya ligi ya klabu bingwa barani Afrika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Ngaya ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia Zahir Mohammed katika dakika ya 19 ya mchezo huo huku goli la kusawazisha la Yanga likifungwa na Haji Mwinyi katika dakika 43.

Kipindi cha pili, timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu na kosa kosa zikawa za pande zote mbili.

Yanga inafuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-2, baada ya Jumapili iliyopita kushinda 5-1 ugenini mjini Moroni nchini Comoro.

Mchezo huo uliochezeshwa na marefa Alex Muhabi, washika vibendera Ronald Katenya na Lee Okello.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *