Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC leo inashuka dimbani dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye mechi ya mwisho kombe la shirikisho Afrika kundi A.
Yanga inacheza mechi hiyo ili kukamilisha ratiba kwasababu haina nafasi ya kuvuzu hatua ya nusu fainali baada ya kuambulia alama 4 katika michezo mitano iliyocheza mpaka sasa.
TP Mazembe inaongoza kundi hilo ikiwa ana alama 10 katika michezo mitano iliyocheza ikifuatiwa na Medeama ya Ghana ambayo imejikusanyia alama nane na MO Bejaia ina alama tano huku Yanga ikishika mkia kwa kuwa na alama nne tu.
Yanga jana ilifanya mazoezi yake ya mwisho jijini Lubumbashi kwa ajili ya mechi hiyo ya kukamilisha ratiba ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Katika mechi ya kwanza iliyofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Yanga ilifungwa 1-0 dhidi ya TP Mazembe na leo wanarudiana katika mji wa Lubumshi.