Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga huenda bado ina nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Afrika baada ya TP Mazembe kutoka 0-0 dhidi ya MO Bejaia kwenye mechi ya Kundi A ya michuano hiyo iliyofanyika katika uwanja wa United Maghrebine mjini Bejaia.
Baada ya matokeo hayo TP Mazembe inaongoza kundi A ikiwa na alama saba, MO Bejaia alama tano, Medeama alama mbili huku Yanga ikiwa na alama moja ambapo kila timu imecheza mechi tatu hadi sasa.
TP Mazembe ina nafasi kubwa ya kuingia nusu fainali ya michuano hiyo kutokana na kukusanya alama saba huku nafasi ya pili ikionekana kuwa wazi kwa timu zote tatu zilizosalia.
Yanga wanatarajia kurudiana na Medeama julai 26 nchini Ghana huku TP Mazembe wakicheza na MO Bejaia Julai 27 jijini Lubumbashi.