Yamoto Band wapo jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania kwenye msimu wa nne wa Coke Studio Africa.
Yamoto Band wataonekana kwa mara ya kwanza kwenye show hiyo mwaka huu kwa kushirikiana na msanii wa Ethiopia anayeitwa Lij Michael aliyeimba wimbo wa ‘Zaraye yehun nege’.
Lij Michael ambaye pia anashiriki kwa mara ya kwanza kwenye msimu wa nne wa Coke Studio Africa unaofanyika nchini Kenya.
Yamoto Band wanatarajiwa kujumuisha ladha za Bongo na vile vya hip hop ya Ethiopia huku wimbo wao ukitayarishwa na producer wa Ufaransa, DSK mwenye asili ya Ivory Coast.
Enock Bella amesema wanaishukuru Coke Studio Africa kwa kuwaamini na kuwapa fursa kushiriki kwenye kipindi kuonesha uwezo wao wa kimuziki kwenye show hiyo kubwa Afrika Mashariki.
Pia ameongeza kwa kusema wanafurahia kufanya kazi na Lij Michael na wanategemea kuchanganya muziki wa Bongo Fleva na muziki kutoka Ethiopia.
Kwa upande wake Lij Michael aliisifia Coke Studio Africa akidai kuwa mabadilishano kati ya Yamoto Band na yeye ni ya kupendeza.