Wiki iliyopita Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepitisha mabadilko ya Katiba ya Chama hicho kwenye mkutano mkuu maalum uliofanyika katika ukumbi wa Dodoma Convetion Center sasa Jakaya Kikwete Hall.

Mabadiliko hayo yaliyofanywa na Chama hicho kwenye mkutano huo ni kama ifuatavyo.

  1. Wajumbe wa NEC watakuwa wanatokana na Mikoa na si wilaya kama ilivyokua awali. Kwa hiyo kila mkoa utakuwa na MNEC mmoja. Utaratibu wa kuwa na wajumbe wa NEC kutoka kila wilaya umefutwa.
  1. Makatibu wa Fedha na Uchumi (wa mikoa na wilaya) wamefutwa.
  1. Makatibu Wasaidizi (wa mikoa na wilaya) wamefutwa.
  1. Wajumbe wawili wa kuchaguliwa kwenye Kamati za Siasa (za mikoa na wilaya) wamefutwa.
  1. Shirikisho la Vyuo vikuu au mkoa wa vyuo vikuu wa CCM ambao ulikua taasisi inayojitegemea, kuanzia sasa itakuwa idara ya UVCCM, na itawajibika chini ya UVCCM.
  1. Wajumbe wa Kamati kuu (CC) wamepunguzwa kutoka 34 hadi 24.
  1. Wajumbe wa NEC wamepungua kutoka 388 hadi 163 watu 225 wamepunguzwa .
  1. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wamepungua kutoka 2,380 hadi 1,706 watu 764 wamepunguzwa.
  1. Rais aliyeko madarakani ataruhusiwa kugombea kipindi cha pili mfululizo bila kupingwa ndani ya chama.

10. Kura za maoni za wabunge zitapigwa na Mkutano Mkuu wa Jimbo, na za Madiwani zitapigwa na Mkutano Mkuu wa Kata na sio wanachama wote kama ilivyokua awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *