Rais wa Gambia, Yahya Jammeh amekubali kung’atuka na kuondoka nchini humo baada ya kushauriwa na viongozi wa Ukanda wa Magharibi.

Adama Barrow ambaye ndiyo mshindi wa kiti cha urais nchini humo ametangaza hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter, baada ya mazungumzo ya saa kadha yaliyonuiwa kumshawishi Bw Jammeh kukubali matokeo ya uchaguzi.

Mataifa ya Afrika Magharibi yamewatuma wanajeshi Gambia na kutishia kumuondoa Jammeh madarakani kwa nguvu.

Barrow amepishwa kuwa rais mpya wa Gambia katika ubalozi wa Gambia mjini Dakar mnamo Alhamisi.

Jammeh alikuwa amepewa muda kuondoka madarakani kufikia saa sita mchana la sivyo aondolewe kwa nguvu na wanajeshi wanaoungwa mkono na UMoja wa Mataifa.

Muda rasmi wa wa Yahya Jammeh kuongoza kikatiba ulifikia kikomo siku ya Jumatano lakini alikataa kuondoka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *