Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu amesema utaratibu wa upimaji wa kifua kikuu na Ukimwi bar kwa bar sio wa lazima, ila watatumia ushawishi kuhakikisha wananchi wanapima na kujua afya zao.

Ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi (NACP).

Amesema kuwa ”Tutatekeleza mpango wetu wa kupima TB na Ukimwi kwenye bar ila hautakuwa wa lazima, tutakachofanya ni kuwashawishi wananchi kutumia fursa ya kusogezewa huduma hiyo”.

Aidha ameongezea kuwa Wizara ipo katika mkakati wa kubadilisha sera na sheria za Ukimwi na kuruhusu mtu aweze kujipimwa mwenyewe na kutoa fursa kwa vijana kuanzia miaka 15 kujipima wenyewe bila ridhaa ya wazazi.

Hatua hizo ni kufuatia serikali kutaka kubainisha na kuwatambua watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi pamoja na TB.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *