Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa hajawahi kuumia kuachana na mwanaume yoyote katika maisha yake.
Wolper amesema kuwa alikuwa na kawaida ya kuwaanika wanaume aliokuwa akiingia nao kwenye uhusiano ili watu wote wajue akidhani itakuwa ngumu kusalitiwa lakini ikawa kinyume chake.
Muigizaji huyo ambaye kwasasa ni mfanyabiashara amesema kuwa jambo ambalo hajawahi kujutia au kuumia kwa kuwa akiachana na mtu anaangalia waliopo kwenye foleni anachangua tu anayemtaka.
Amesema kuwa “Sijawahi kuumia kuachana na mwanaume ila kinachoniumiza sana ni kwa nini nilimtangaza watu wakamjua ndiyo maana kwa sasa sitaki tena kumtangaza niliyenaye.
Muigizaji huyo aliwahi kutoka kimapenzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ila kwasasa wameachana.