Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper amewajia watu wanaomsema kuhusu pengo lake lilivyokuwa jeusi.
Wolper aliwaacha watu wengi midomo wazi baada ya kuandika maneno hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Sakata hilo lilianzia kwenye mtandao wa Snapchat ambapo mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Husna Maulid kuweka picha ya pengo la Wolper na kumcheka kwa kebehi.
Baada ya kuona hivyo Wolper alimjibu Husna kwa kumuita skeleton kutokana na wembamba wake kwa kuandika
Wolper ameanza kuandika “Walahi nimecheka mpaka nimepaliwa skeleton unajua kuniua mbavu zangu, nalipenda sana pengo langu aaah najua kinachokuumiza hujatia sign….Hapa kazi tu skeleton”.
Pia ameongeza kwa kuandika “Ngoja niwaelezeni kitu kimoja ambacho hamkijui kuhusiana na hili pengo….hili pengo nimelipandia ndege kwenda South Africa kwenda kulitoa na kuweka ma silver sasa wewe kunguni unatokea pasipojulikana unakuja kuedit ukadhani nitakasirika am soleee…mimi najipenda nilivyo na ikitokea nimechoka nitanyanyua makalio yangu na kwendaa kuweka jino ili niwe na jino so pliz usitokwe nadamu pliz pengo langu ndilo ninalodanga kwa taarifa yako kama ulikuwa hujui”.
Muigizaji huyo ambaye kwasasa amejikita kwenye ujasiliamali kwa kufanya biashara ya maduka ya nguo jijini Dar es Salaam.