Muigizaji wa Bongo Movies, Jacquiline Wolper amesema kuwa kwa sasa anashindwa kumtambua mtoto wake atakaa kwenye sekta gani ingawa bado anamuona mpole sana ila akitaka kuwa staa yeye hana pingamizi.
Wolper amefanikia kuwa mtoto wa kiume ambapo amesema kuwa endapo mtu yoyote akimuongelea vibaya kuhusu mtoto wake atamfungulia mashtaka.
Kuhusu ratiba zake kubadilika ameeleza kuwa ratiba zake zimebadilika kwa kiasi kikubwa sana na yote ni kwa sababu ya mtoto.
Kuhusu suala la tuzo amewaomba waandaaji watoe tuzo kwa usawa na sio upendeleo kama tuzo zilizopita ambazo zilizua mijadala mikubwa sana kwani huwa zinapunguza heshima kwa baadhi ya wasanii.