Mkali kutoka Nigeria, Wizkid usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kushinda tuzo ya MTV Europe Music Awards (EMA) katika kipengele cha Best African Act zilizofanyika Rotterdam nchini Uholanzi.
Wasanii wengine aliokuwa wakiwania tuzo hiyo ni pamoja na Alikiba wa Tanzania, Olamide kutoka Nigeria na Black Coffee na Cassper Nyovest wa Afrika Kusini.
Huu ni mwaka wa pili kwa waandaaji wa tuzo hizo kukiweka kipengele hicho ambacho kitamfanya Wizkid kuingia kwenye hatua nyingine ya kuwania tuzo ya ‘Best Worldwide Act Africa/India’ ambayo mwaka jana ilichukuliwa na Diamond Platnumz baada ya kumwaga Priyanka Chopra aliyewahi kuwa Miss World mwaka 2000.
Vile vile mwanamuziki huyo amefanikiwa kushinda tuzo ya Afrika katika kipengele cha mwanamuziki bora wa mwaka ambapo tuzo hioz zimefanyika Lagosi nchini Nigeria usiku wa kuamakia leo.
Wizkid ameonekana kufanya vizuri zaidi mwaka huu kutokana na kushinda tuzo kibao wakati akifanya hivyo kwenye tuzo za MTV MAMA aliposhinda tuzo nne kwa mpigo.