Mwanamuziki nyota wa Nigeria, Wizkid ameachia rasmi album yake ya nne iitwayo “Made in Lagos” ambapo mastaa mbali wamesikika katika albamu hiyo yenye ngoma 14.

Mbali na yeye pia albamu hiyo itakuwa na mastaa kama H.E.R, Burna Boy, Damian Marley, Temi na wengine wengi.

Ikiwa ni masaa matano tu toka kuachiwa kwake imeweka rekodi kwenye mtandao wa AudioMack kwa kusikilizwa mara Milioni Moja ndani ya masaa hayo

Album hiyo ilitakiwa kuwahi kutoka ila kutoka na maandamano yaliyokuwa yakiendelea nchini Nigeria alilazimika kuchelewa kuachia kazi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *