Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashairiki, Mindi Kasiga, amesema kuwa madereva 21 watanzania wametekwa nchini Congo wakiwa wanelekea katika mgodi wa dhahabu wa Namoyo katika jimbo la Mainiema unaomilikiwa na kampuni ya Banro Gold ya Canada.
Amesema kati ya madereva 24 waliotekwa, 21 ni Watanzania na 3 ni Wakenya hivyo Serikali inafanya jitihada za kuwaokoa madevera hao.
Mindi amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini DRC, madereva hao wametekwa na waasi wa kikundi cha Mai Mai, kilishambulia msafara wa malori hayo uliokuwa ukisindikizwa na askari wa jeshi la DRC (FARDC) na kufanikiwa kupora mali zao zote zikiwemo fedha na kuharibu malori hayo.
Amesema hadi sasa Serikali kupitia Ubalozi wake nchini DRC umechukua hatua kadhaa kuhakikisha madereva hao wanapatikana na wakiwa salama.