Aliyekuwa mke wa Rais wa kwanza wa Afrika Kusini na mpingaji ubaguzi wa rangi nchini Winnie Madikizela-Mandela, amelazwa hospitalii kwa ajili kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.

Familia yake imesema kuwa alipelekwa hospitali ya Milpark mjini Johannesburg kwa ajili ya matibabu.

Disemba mwaka uliopita, Bi Madikizela-Mandela alilazwa hospitali hiyo lakini kile kilichosababisha alazwe hakikutajwa.

Msemaji wake Victor Dlamini amesema kuwa alikuwa ameenda kufanyiwa uchunguzi wa kawaida lakini madaktari wakaamua kumlaza.

Bi Madikizela-Mandela alikuwa mke wa Nelson Mandela, na alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi kusajiliwa kama mhudumu wa kijamii nchini Afrika Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *