Video ya Wimbo wa ‘Acha Niongee’ wa mwanamuziki, Nay wa Mitego umefutwa kwenye Mtandao wa YouTube siku moja baada ya kuachiwa rasmi kwenye mtandao huo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mtandao wa YouTube, video hiyo imefutwa kutokana na madai ya hatimiliki ambayo yamepelekwa huko YouTube na mtu waliyemtaja kwa jina la Rashidi Said Madega.

Uamuzi huo wa YouTube unakuja saa kadhaa baada ya msanii Bright kudai kuwa Nay ameiba mdundo wa ngoma hiyo ambayo walitakiwa kufanya pamoja, lakini baadaye Nay alibadilisha uamuzi na alitaka kufanya ngoma hiyo na Roma badala ya Bright.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bright ameandika; “Wewe ndiye tajiri unayepokonya kidogo cha maskini kuweka mifukoni mwako Mungu utalipa yote uliyoyafanya kwenye muziki wangu nadili na wewe.

Huyu ni mwizi wa beat yangu ambayo nimeipiga mimi na nilimcheki nifanye naye wimbo (collaboration) akaleta tamaa huo wimbo wangu na beat yangu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *