Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego ameshindwa kuachia wimbo wake mpya ‘Mama’ baada ya wimbo huo kupitia Baraza la Sanaa Taifa ‘BASATA’.

Nay ambaye jina lake kamili ni Emanuel Eribarik alitoa taarifa ya kushindwa kuachia wimbo huo kupitia ukurasa wake w Instagram ambapo alipanga kuuachia jana Mei 3 2021.

Nay wa Mitego kupitia ukurasa wake wa instagram amefunguka wimbo wake wa MAMA kupigwa chini na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Ameanza kwa kuandika “Leo Ilibidi Nitoe Wimbo Wa Mama Kama Ambavyo Niliwaahidi Lakini Imekua ngumu kutoa nimeupeleka Basata wameukataa wameniambia una ukakasi unaitaji marekebisho.

Pia ameendelea kwa kuandika na mimi kwa upande wangu siwezi kubadilisha sababu mpk sasa gharama nilizo tumia ni kubwa sana na video ipo tayari kwa hiyo sitoweza tena kuutoa huo wimbo” -Nay wa Mitego

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *