UKO WAPI NIKUFUATE NIAMBIA NIPAJUE ANGALAU NIKUONE…………

What happened to Ray C? What is going on with her life? Who/what is behind all this? Is it all about drugs?

Moja kati ya mashairi matamu ya Ray C yaliyowahi kuandikwa kwenye nyimbo zake ni:

Najiuliza kila siku wapi pa kukutafuta, ni miaka mingi sana hatujaonana
Napata shida sana, nataka niwe nawe, nitakupataje pataje nawe huonekani,
Uko wapi niambie, Uko wapi nieleze, hata kwa barua pepe, au simu ya mkononi…….
Yeyote aliyeimbiwa wimbo huu, kama yuko hai, ajue wakati halisi wa yeye kuwa anatafutwa na Ray C ni sasa!! Ray C anamtafuta huyo mtu DESPERATELY!!

Kwanini? Siku moja Ray C aliwahi kuulizwa kuhusu maudhui ya nyimbo hiyo na kuulizwa kuwa ni nani hasa aliyekuwa mlengwa wa mashairi hayo na maelezo yake hayakuendana kabisa na walichokitarajia mashabiki, Ray C alimtaja baba yake.

Wakati mashabiki wakidhani alikuwa amezama kwenye dimbwi la mahaba na mwanaume anayetamani waishi nae maisha ya mume na mke, kwake mashairi hayo yalikuwa na ujumbe mzito sana, yalikuwa ni zaidi ya uhusiano wa kawaida, ulikuwa ni uhusiano wenye maana kubwa sana kwenye maisha yake na ndio maana nadiriki kusema kuwa aliyeimbiwa wimbo huo (kama yuko hai) AJITOKEZE ili ndoto ya Ray C itimie.

Huyo mtu ni tiba kwa maradhi ya Ray C, ni ponyo ambalo sio rahisi watu kulifahamu ni suluhisho la matatizo mengi ambayo yanamkuta Ray C leo.

Baada ya kusambaa kwa video inayomuonyesha mrembo huyo na staa mkubwa wa zamani kwenye Bongo Fleva akipiga kelele kama mtu aliyerukwa na akili ni wazi kuwa tiba ya Ray C ni tofauti sana na tiba ambazo watu wanafikiria.

Wanasaikolojia wanaweza sana kumsaidia Ray C kuliko ambavyo watu wanafahamu.

Ni wakati wa Ray C kukumbushwa kuhusu Rehema Chalamila, ni wakati wa Ray C kukutanishwa na rafiki zake wa utotoni, kupelekwa kwenye maeneo ambayo alikuwa akipenda na kufurahia kwenda alipokuwa mtoto.

Ni wakati ambao tiba za vidonge na sindano zinapaswa kupewa nafasi ndogo zaidi kuliko tiba ya saikolojia yake.

Ray C alikuwa akiheshimu baadhi ya watu kwenye familia yake, majirani zake, rafikizake ambao wakimwambia kitu atatii bila shuruti lakini kubwa in kuwa kuna watuambao daima kwake humpa faraja na furaha ya kweli, sio faraja au furaha inayotokana na mali na anasa.

Wazazi wake, ndugu zake na marafiki kadhaa miongoni mwa marafiki zake ni watuambao LAZIMA at some point walikuwa ndio THAMANI ya maisha yake.

What happened to the whole life you have loved so dearly Ray C?

Please comeback again, forget everything you have been through…….you are more than drug addicted female artist. You are Chalamila’s lovely daughter, an angel to your parents’ eyes!! Please wake up and start over!! Ray C please!! No more drugs, no more pain, no life miserable life!! Please BE OUR SHINING STAR AGAIN!!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *