Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema klabu ya Manchester City bado ina kazi ngumu ya kuifikia rekodi ya timu yake ya msimu wa 2003/04 ilipomaliza ligi bila kufungwa.
Wenger amekiri kuwa Manchester City wana timu nzuri na wanafanya vizuri lakini ni vigumu kurudia rekodi hiyo katika miaka ya sasa ambapo mazingira ni mazuri zaidi kwa timu zote kuanzia bajeti ya usajili hadi maandalizi.
Amesema kuwa “Ni timu nzuri na wanacheza soka la kuvutia lakini ni mapema kutoa utabiri kama watafikia rekodi ya Arsenal kutokana na kila timu kuwa na uwezo wa kufanya maandalizi mazuri”,
Aidha Wenger ameongeza kuwa ni mapema sana kusema hivyo huku akikumbushia namna ambavyo Real Madrid ilikuwa inaelezwa miezi michache iliyopita na hali inayokutana nayo hivi sasa ya kupoteza mechi mbili mfululizo.
Wenger amemaliza kwa kusema anamuheshimu kocha Pep Guardiola hivyo hapendi sana kuongea kuhusu timu yake kwnai yeye pia hafanyi hivyo. Manchester City na Arsenal zinakutana wakati Man City ikiongoza ligi kwa alama 28 na Asernal ikiwa na alama 19 katika nafasi ya tano.