Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa anatamani kuifundisha timu ya taifa ya Uingereza kwa siku za baadae lakini kwasasa ataendelea kubaki katika klabu yake.

Wenger amesema anatamani kuifundisha Uingereza kwa siku za mbele kutokana na watu wake wa karibu kumshawishi kuchukua timu hiyo.

Wenger mwenye umri wa miaka 66 kesho anatarajia kusheherekea miaka 20 tangu aanze kuifundisha Arsenal wakati huo mkataba wake ukimalizika mwisho wa msimu huu.

Chama cha Soka nchini Uingereza (FA) kinatafuta kocha mpya kufuatia kuondolewa kwa Sam Allardyce kutokana na kukumbwa na kashfa ya usajili baada ya uchunguzi uliofanywa na gazeti la Telegraph.

Big Sam aliyerithi mikoba ya Roy Hodgson amedumu kwenye timu hiyo kwa siku 67 kabla ya kutimulia wiki hii ambapo ameiongoza Uingereza kwenye mechi moja dhidi ya Slovakia na kushinda 1-0.

Timu hiyo kwasasa inaongozwa na kocha wa Gareth Southgate ambaye ataiongoza katika michezo minne kabla ya kupatikana na kocha kamili, mechi za Uingereza zitakazoongozwa na Southgate dhidi ya Malta Oktoba 8, Slovenia Oktoba 11, Scotland Novemba 11 November pamoja na mechi ya kirafiki dhidi ya Uhispania Novemba 15.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *