Si unakumbuka mwaka jana wakati wa Birthday ya Wema ambapo mama yake Diamond Platnumz aliweka picha ya staa huyo mtandaoni na kumpongeza?

Lakini unakumbuka tena kuwa bi. Mkubwa huyo hakufanya hivyo kwa mka-mwana wake Zari a.k.a Boss Lady na kupelekea kuibuka kwa minong’ono?

Unakumbuka kipindi cha nyuma zaidi, Zari a.k.a Mama Tiffah na Wema walikuwa kwenye mgogoro wa moja kwa moja ikiwemo kutupiana vijembe mtandaoni huku kukitengenezwa ‘team Wema na team Zari’ kwaajili ya kusapoti ‘wawapendao’?

Waswahili husema, ‘Wawili wakigombana, shika jembe ukalime’; unajua kwanini ni muhimu kuzingatia msemo huo?

Ni kwasababu Wema Sepetu ‘amekula shavu’ la mualiko wa kuhudhuria shughuli ya AROBAINI ya mtoto wa Zari na Diamond Platnumz, Prince NILLAN.

Shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika kesho.

Nillan alizaliwa tarehe 6 Disemba 2016 hivyo siku ya Jumamosi atakuwa anatimiza siku 65 ingawa atakuwa anasherehekea shuguli ya 40.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *