Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa kama ikitokea akiacha na mpenzi wake wa sasa Whozu basi ataweza kujinyonga.

Wema amesema kuwa, pamoja na kwamba hakujiua kwenye uhusiano wake wa kimapenzi huko nyuma likiwemo penzi la msanii Diamond Platnumz na wengineo, lakini safari hii akiachwa na Whozu ataweza kujinyonga.

 Wema amesema kuwa, kama akiachwa na Whozu, basi watu wakaribie msibani kwa ajili ya kumzika kwa sababu jamaa huyo amemuheshimisha mno.

Penzi la Wema na Whozu limechipuka kipindi cha hivi karibuni na limeanza kuteka mazungumzo mtandaoni.

Wema anasema kuwa, pamoja na kwamba watu wanambeza kuwa, lakini anataka aachwe na maisha yake kwani ukweli ni kwamba amezama kabisa kwenye dimbwi la mahaba na ana furaha mno.

Penzi la Wema na Whozu halikuanza leo wala jana kwani walijificha kwenye mwavuli wa marafiki, ila walikuwa wakifanya kwa siri kabla ya kuamua kujitokeza hadharani kama wapenzi baada ya Whozu kuachana na mzazi mwenzake, Tunda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *