Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na kusema pamoja na mashabiki wake kumsema baada ya yeye kumuanika mpenzi wake lakini yeye ndio amemchagua.
Kauli hiyo imekuja baada ya mashabiki kumshambulia katika mitandao ya kijamii baada ya kumtambulisha mpenzi wake mpya ambaye mwenye amesema kuwa ni mumewe mtarajiwa.
Wiki iliyopita Wema alizua gumzo baada ya kuanika picha Mtandaoni akiwa na mpenzi wake amayejulikna kama Patrick Christopher ‘PCK’ ambapo mashabiki zake wengi walionekana kuchukizwa na Mahusiano hayo.
Wema amesema kuwa yeye ana uamuzi wake binafsi wa kufanya anachotaka kwenye maisha yake, lakini anashangaa watu wengine wanamuingilia mpaka kwenye maisha yake binafsi na kutokwa povu.
Watu wengi wamejitokeza na kumshauri Wema aachane na yule mwanaume kwani haendani naye hata kidogo jambo ambalo limeonekana kumkera Wema.