Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa amepata dili na kampuni ya usambazaji wa filamu nchini Agusta kwa ajili ya kusambaza filamu yake ya ‘Heave Sent’.
Wema Sepetu amesema kuwa amesainishwa mkataba na kampuni mpya ya kusambaza filamu za Kibongo ya inayoitwa kwa jina la Agusta.
Muigizaji huyo ameishukuru kampuni hiyo kwa kuchukua kazi yake ya Heaven Saint na kumlipa donge nono, jambo ambalo limemfanya kuzidi kuendelea kufanya kazi nzuri.
Amesema kuwa Kwanza nina furaha sana kuchukua tuzo ambayo ninajua kabisa imenipa heshima ya kutosha.
Wema Sepetu alishinda Tuzo ya Msanii Bora wa Kike 2018 zilizokuwa zikitolewa na Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.