Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amesema kuwa anatamani kuishi na Kairo, ambaye ni mtoto wa Happiness Magese.

Wema alionyesha hisia hizo kupitia moja ya ukurasa wa kijamii wa Magese, baada ya dakika chache kutupia picha ya mtoto wake.

“Da Happy ukija si utanigaia huyu apa hata siku tatu, naomba tafadhali, ila sijui maana huyu ni zaidi ya roho kwako, aaah mimi nitakuja kukaa na wewe tu hata wiki ili nimng’ate ng’ate mashavu,” aliandika Wema.

Baada ya ujumbe huo, Magese aliibuka na kumjibu Wema kwa kumsihi asikate tamaa badala yake awe na subira kwani siku moja Mungu atamfanyia maajabu na yeye aitwe mama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *