Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amshukuru mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kumtia moyo katika kazi zake za Sanaa.
Wema amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika “Picha ya hapo juu uliyoomba ni mmiliki halali wa Filamu ya Heaven Sent ambaye kajisajili Cosota na Bodi ya Filamu, anazo haki miliki zake zote na ndio aliyeshinda Best Actress 2018 kwa kuwa amekidhi sababu zote za kuwa Mshindi,”.
Kauli ya Wema inakuja mara baada ya RC Makonda kumtaka muigizaji huyo kuweka picha ya tuzo aliyoshinda katika ukurasa wake wa Instagram baada ya baadhi ya watu kujitokeza na kukosoa tuzo hizo.
Wema ameendelea kwa kusema anataka tasnia ya Filamu iwe na watu wenye kujielewa na wenye upeo mkubwa, sio wenye kukurupuka na kuvamia jambo bila kudadavua na kujua ni kitu gani kinatakiwa kufanyika.
“Yote yanawezekana, wasanii ni watu wenye wadhifa mkubwa sana, najivunia kuwa mmoja kati yao. Ninajua hata wewe unajivunia kuwa kati yetu sisi ukiwa kama Mlezi ukituongoza kila leo kutaka tufike sehemu nzuri na Inshallah tutafika,” ameeleza Wema
“Lakini pia naomba nikuahidi, sitokuangusha maana kumuangusha RC wako nako sio pambe kabisa,”.