Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amesema kuwa yupo tayari kuolewa kwa mahali ya kawaida kwani hataki zile mahari kubwakubwa wanazotaka baadhi ya mastaa za shilingi milioni mia tano.
Kauli hiyo ya Wema ameitoa baada ya kuibuka histori kuwa mrembo huyo yupo mbioni kufunga ndoa japokuwa mwenyewe hajaweza wazi suala hilo.
Wema amekiri kuwa kwenye uhusiano huo wa kimapenzi na mwanaume ambaye jina na sura yake vimewekwa kwenye mabano hadi atakapomalizana na familia ya mrembo huyo juu ya suala hilo la mahari.
Wema amesema kuwa ” Hapana, mimi siwezi kusema nataka milioni mia tano, vyovyote atakavyokubaliana na familia yangu ndivyo hivyo,”.
Muigizaji huyo kwasasa yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume ambaye amekataa kutaja jina lake kuhofia kumtangaza mwanaume katika vyombo vya habari.