Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ametoa ya moyoni kuhusu uhusiano wake na Whozu na uwezekano wa kufunga naye ndoa.
Wema ameweka wazi kwamba, kwamba hayupo tayari hata kidogo kuingia kwenye ndoa na Whozu kama ambavyo imetabiriwa na wengi kuwa hakuna ndoa hapa!
Wema amesema kuwa, huo ndiyo ukweli wake kwamba, hayupo tayari kabisa kuolewa na Whozu, na kuwaacha wengi wakijiuliza kama uhusiano wake na kijana huyo wa watu bado upo imara au ndiyo mwanzo wa nyufa kuanza kujitokeza.
Itakumbukwa kuwa, Wema Whozu walianza uhusiano wao takriban mwezi mmoja uliopita na wamekuwa wakipigwa vita mitandaoni ambapo wengi wanasema Wema anajidhalilisha kuingia kwenye uhusiano na Whozu ambaye wengi walimtaja kama mdogo si tu kiumri tu, bali pia kiumaarufu.
Wiki mbili zilizopita, Whozu alimpeleka Wema kisiwani Zanzibar kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo walijiachia kimahaba na kula bata aliyenona.
Ndani ya muda mfupi inashangaza kwa Wema kusema kwamba uhusiano wake na Whozu si wa muda mrefu na katu hautakuja kudumu.