Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka juu ya kukubalika na mama mzazi wa mpenzi wake wa sasa ambaye Whozu.

Baada ya Wema kuthibitisha kuwa kwenye penzi zito na Whozu huku wakijiita Chimama na Chibaba, kuliibuka habari za mitandaoni kwamba familia ya Whozu akiwemo mama yake hawataki kabisa kusikia habari za mtoto wao kutoka kimapenzi na mlimbwende huyo.

Habari hizo zilidai kuwa, familia hiyo inamkubali mno video vixen Tunda ambaye amezaa na Whozu huku wakimuona Wema ni mkubwa kwa Whozu.

Wema amesema kuwa, mama Whozu anampenda na kumkubali kama ambavyo na yeye anampenda na kumkubali.

“Kitu kimoja ambacho naweza kukisema ni kwamba mama mkwe ninampenda na ananipenda hivyo tu,” anasema Wema na kuongeza;

“Nimepitia maisha mengi sana, nimepitia maisha ya kusimangwa, ikafika muda nikaona kama nimekata tamaa, lakini kwa sasa hivi sina msongo wa mawazo, mbona kwa sasa hivi nipo sawa sana?

“Sihitaji msaada wa mtu yeyote tena nasema sihitaji msaada wa mtu yeyote, kwa sasa nipo sawa sawia,” anasema Wema ambaye penzi lake na Whozu limekolea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *