Staa wa filamu nchini, Wema Sepetu ni mmoja wa watu maarufu waliohudhuria hafla ya utambulisho wa mwanamuziki mpya wa WCB, Maromboso.
Wema Sepetu amesema kuwa alipigia simu na aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz kuhudhuria utambulisho huo uliofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam.
Muigizaji huyo amesema kuwa kwakua hakuna tatizo na Diamond ameamua kuhudhuria hafla hiyo pamoja na mastaa wengine wa Bongo ili kumpa sapoti.
Maromboso anakuwa mwanamuziki wa sita kujiunga na WCB baada ya Harmonize, Rayvanny, Rich Mavoko, Queen Darleen na Lavalava.