Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa ataendelea kung’ara hata kama akizeeka na kuwa kikongwe kisha kuaga dunia.

Wema amesema kuwa, nyota yake itaendelea kung’aa siku zote wala haitafifia kama baadhi ya watu wanavyotamani iwe kwani amezaliwa nayo na atazikwa nayo na akiwa kaburini bado ataendelea kuzungumzwa.

“Hata kama watu wataichafua kiasi gani, nyota yangu itaendelea kung’aa hadi nitakapokuwa mzee. Nitakuwa ni bibi mwenye mvuto na hata nikifa bado watu watataka kunizungumzia na kusikiliza hadithi zangu,” anasema Wema.

Pia Wema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjaalia nyota hiyo ambayo inawezekana kuna watu wanatamani izimike wakati wowote, jambo ambalo haliwezekani leo wala kesho na kwa kuwa alitoka nayo tumboni kwa mama yake, Miriam Sepetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *