Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na kuongelea uhusiano wake na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto huku akidai kuwa ni mdogo wake ila mazoea yalizidi hivyo aliamua kumuweka kando.

 Siku za nyuma Wema na Hamisa walikuwa marafiki sana kwa miaka mingi na hata ni mara nyingi Hamisa amekuwa akisikika akimuita Wema dada yake.

Wema amesema kuwa Mimi hamisa ni kama mdogo wangu, hivyo yaani waga nasema kila siku Lakini sometimes mazoea yakizidi sana sijui huwa inaleta mushkeri kwaiyo inabidi kila mtu abaki kwenye mipaka yake ili ajue hapa natakiwa nipitilize au hapa nisipitilize”.

Watu wengi walihusisha Wema kugombana na Hamisa na Diamond lakini Wema aliweka wazi kuwa aligombana na Hamisa kwa sababu alimsikia anamsema vibaya kwa watu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *