Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa hana bifu na wasanii wenzake Irene Uwoya na Lulu licha ya kutokuwa karibu kama zamani.
Taarifa za awali zinasema kuwa Irene Uwoya na Lulu walifika nyumbani kwa Wema Sepetu wakiwa na wasanii wenzao ambao ni Aunt Ezekiel, Jackline Wolper pamoja na Kajala ambao walikwenda kama wasuluhishi.
Pampja nao waliwashirikisha viongozi wa wasanii hao (managers) ambaye ni Martin Kadinda pamoja na Aloy.
Inaelezwa kuwa kwa kipindi kirefu Wema na Lulu wamekuwa hawana maelewano mazuri kutokana na sababu ambazo hazijawekwa wazi huku kwa upande wa Irene Uwoya suala la kashfa zilizotolewa na mpambe wake “Aristoste’ dhidi ya Wema zikitajwa kama moja ya sababu iliyosababisha kukosekana kwa maelewano baina yao.
Mpaka sasa bado taarifa za ndani zaidi kuhusu marumbano ya nyota hao hazijawekwa wazi licha ya kuenea kwa video inayoonesha sehemu ya mazungumzo mpaka hatua za kuzuka kwa mgogoro huo uliopo.