Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amekanusha kutoka kimapenzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja ambaye ni mume wa muigizaji mwenzake Irene Uwoya.
Kauli ya muigizaji huyo imekuja baada ya kusambaa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa alitoka kimapenzi na Dogo Jana ambaye ni mume wa rafiki yake Irene Uwoya kitu ambacho amekanusha vikali.
Wema amesema kuwa habari hizo zinasambazwa kwa ajili ya kumchafua yeye na mpenzi wake aliyemtambulisha hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii.
Taarifa hizo zinasema kuwa Dogo Janja na Wema Sepetu walitoka kimapenzi ambao walikutana mkoani Arusha na kufanya yao kitu ambacho Wema amesema kuwa siyo kweli.
Kwa upande wa Dogo Janja bado hajazungumzia kuhusu tuhuma hizo zinazolenga kuichafua ndoa yake na Irene Uwoya ambayo inaonekana kutikisika hivi karibuni.
Dogo Janja na Irene Uwoya walifunga ndoa mwaka jana ambapo hadi sasa wapo kwenye ndoa japokuwa wamekuwa na migogoro ndani ya ndoa hiyo.